Kamanda
wa Polisi Mkoa wa Dodoma, Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID
MISIME akiongoza waombolezaji kuaga miili ya Askari Polisi waliofariki
katika ajali ya gari.
Waombolezaji.
Miili ya Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ikiwa imebebwa.
Askari Polisi waliofariki katika ajali ya gari ya kugongana uso kwa uso na basi la Mohamed Trans wameagwa jana Mkoani Dodoma tayari kwa mazishi.
Akiongea
kwa masikitiko Kamishna Msaidi Mwandamizi wa Polisi DAVID MISIME
amewashukuru watu waliojitokeza kuungana pamoja kuaga miili ya Askari
hao.
Pia
amewataka madereva wote kuwa waangalifu wanapokuwa wanaendesha vyombo
vya moto na kuzingatia sheria za usalama barabarani ili kuepuka ajali
zinazoweza kujitokeza za namna hii.