Mapunda
alisema: "Mimi huwa nina mikakati ninapokuwa uwanjani, nataka kuona
wachezaji wenzangu wakiwa makini na kuendana na jinsi mpira
unavyochezwa.
"Saa
nyingine wanajisahau na ni haki yangu kuwakumbusha ingawa wanatafsiri
kuwa mimi ni mkali lakini ina faida kwani mwishowe timu inapofungwa
anayekuwa wa mwisho golini ni mimi," alisema.
"Huwa nakua
mkali kwa mabeki wangu nikitaka wawe makini zaidi kwenye mpira, pia
wakati mwingine mazingira yakiwa magumu huwa nawakumbusha viungo na
washambuliaji kuwa makini kwani wanaiweka timu hatarini kwa kiasi fulani
wasipokuwa makini.
"Unajua
mimi sipendi kufungwa mbali na timu yangu kupoteza mchezo, naamini kama
kina Donald (Mosoti), Owino (Joseph), Kaze (Gilbert) na mabeki wengine
wanakuwa makini basi kila mchezaji ataonekana bora na timu pia
itaonekana bora."
Mara kwa
mara Mapunda amekuwa akiwakaripia wachezaji wenzake hususan wale wa
nafasi za beki na kiungo huku wakati mwingine akiwasukuma akiwataka
wakakabe hususan katika mipira ya kona na adhabu. Chanzo: mwanaspoti