ITV, EATV, Channel Ten, Star TV na vituo vingine vya runinga Tanzania
vimepata mpinzani mwenye nguvu. Ni kituo kipya kiitwacho TV1. Kituo
hicho kinamilikiwa na kampuni ya Sweden iitwayo, Modern Times Group.
Kampuni hiyo iliyojikita zaidi kwenye masuala ya burudani imeanzisha
kituo hicho mapema mwaka huu na kwake ikiwa ni TV ya kwanza ya bure
kuwahi kuianzisha.
TV1 itakuwa ni channel ya burudani itakayokuwa pia mchanganyiko wa
habari zilizoandaliwa nyumbani na za kimataifa pamoja kurusha filamu za
kimataifa na TV series.
Tayari kituo hicho kimeajiri watangazaji mbalimbali wazoefu kufanya
vipindi mbalimbali wakiwemo Marygoreth Richard aliyekuwa msomaji wa
habari za East Africa Radio, Angel Karashani (TPF6) na aliyewahi kuwa
mtangazaji wa Channel Ten, Nzowa
(Picha kwa hisani ya Bongo5)