Roman Abramovich mwenyewe binafsi aliongea na mchezaji wa zamani wa Lille Eden Hazar kumhaidi kumlipa mara 3 ya mshahara aliokuwa akilipwa na klabu ya Ufaransa kama angekubali kujiunga na Chelsea mnamo mwaka 2011, imefahamika.
Mmiliki
huyo wa Chelsea alizungumza na Hazard kwa njia ya simu wakati akiwa
kwenye viwanja vya mazoezi vya klabu ya Ufaransa - mbele ya wachezaji
wenzake wa timu hiyo.
Boss
wa Lille Rudi Garcia - ambaye alimfundisha Hazard wakati huo -
alishuhudia kiteno hicho na ametoa siri hiyo kwenye kitabu chake kipya.
Garcia
anaelezea namna Didier Drogba alivyompigia simu Gervinho na kumuuliza
kama Hazard - ambaye sasa amehamia Chelsea - yupo nae karibu. Gervinho
akajibu: "Ndio, nipo nae hapa."


Hazard akachukua simu na Garcia anasema kwamba Drogba akampa simu Abramovich ambaye akamwambia Hazard: 'Sifahamu unalipwa kiasi gani hapo Lille, lakini nitakulipa mara 3 ya unavyolipwa ukihamia kwenye timu yangu."
Mshambuliaji
huyo wa Ubelgiji, ambaye alihamia Stamford Bridge kwa ada ya uhamisho
wa £32million mnamo mwaka 2012, amekuwa kwenye fomu nzuri akiisadia
Chelsea kushinda mechi muhimu na kuiweka timu hiyo ya Jose Mourinho
katika kilele cha mbio za kugombea ubingwa.