Wednesday, 8 January 2014

UPO KAMA DUME LA BATA FANYA HIVI

MUHALI gani mabibi na mabwana nina imani tumeuanza mwaka vizuri, najua mmenisubiri kwa hamu kutaka kujua nimekuja na mapya gani. Jamani hakuna jipya chini ya jua, zaidi ya kukumbushana tulivyo visahau.
Leo  nami siwezi kuzipunguza raha zenu bali kuziongeza.

Nashukuru kwa wote mlionipongeza kwa kupata mafunzo ambayo hawakuyapata hapo awali, siyo wote wamepitia mafunzo ya utaratibu wa maisha ya jando na unyago.
Kutokana na kupokea maombi ya akina baba ambao huamini nipo kwa ajili ya kuwapendelea akina mama. Ni kweli hii ni kona yetu lakini hatukamiliki bila wao, nao wameomba niwakumbuke katika ufalme wa uhusiano, nami sina hiyana kwa vile wao ndiyo wapiga gitaa sisi wachezaji tu.
Nimekuwa nikikumbana na maswali mazito toka chumbani juu ya matatizo ya uendeshaji wa mashua kwa nahodha kuteremka kabla chombo hakijagota. Hili lilikuwa swali ambalo naamini limekuwa sugu katika nyumba zetu kila kukicha kwa akina baba kupungua uwezo wa kufunga magoli ya mapema na akiishalipata huvua jezi na kujilaza nje ya uwanja.
Hii imekuwa ikiwaumiza sana akima mama, sawa na kipa aliyefanya mazoezi ya kuzuia mashuti makali lakini baada ya mpira kuanza mshambuliaji abaki na kipa akupigie shuti kama mate ya mlevi. Inaudhi kwa kweli, mbaayaaaa eeeh.
Kibaya zaidi anatoka nje ya uwanja na kukuacha ukiteseka na kukimbilia kujikanda na maji ya moto kila siku mwisho kutaota sugu na kuua virutibisho na kuondoa ladha. Japokuwa si mtaalamu sana wa mambo hayo, suala hili lilikuwa la Babu Poa lakini amepata udhuru na siwezi kuliacha lilale.
Kwa vile mimi ni nyani mzee mzoefu wa pori kuna vitu nilikutana navyo ambavyo vilinipa somo na kuona kuna umuhimu wa kuwaeleza na kina baba wengine nao wajaribu kutumia njia hii kama wana matatizo hayo.
Wapo niliowaelekeza na kukubaliana na nilichowafundisha na wakafurahia safari yao. Mmh! Naona mimacho imekutoka na kusubiri ujue ni mbinu gani za kukufanya angalau ulie machozi mawili na kumfurahisha mpenzio.
Siku moja nilikutana na mwanaume mmoja ambaye ukimuangalia utajua hana kasoro yoyote basi kama kawaida tukaingia kwenye shamba lake la minazi. Mwanamke nikaanza kuukwea huku nikitatalika kama bisi jikoni, kijana wa watu Mungu alimjalia sura na uwezo wa kuuyumbisha mnazi wake kimadaha na kufanya nihisi raha ya ajabu.
Nami raha ziligonga kila kona ya kweli na kuzidi kuukwea  kwa kasi kama komba mzoefu wa minazi nikikitafuta kilele. Lakini kabla sijafikia madafu ili ninywe maji yake, alilipasua dafu lake na kuyamwaga maji yake pembeni ambayo nami nilikuwa na kiu nayo pia ndiyo yaliyonifanya niupande mnazi wake kwa kasi.
Nilimshangaa kuumwaga utamu sehemu isiyohusika. Nilijiuliza alikuwa na maana gani? Baada ya muda alinipandisha tena juu ya mnazi wake, kwa vile mzuka ulikuwa haujashuka moto ulianzia ulipoishia. Nilijikuta nikifika mwisho wa mnazi yaani kilele huku mpenzi wangu naye akininywesha maji ya madafu yaliyokuwa matamu kupita kiasi.
Baada ya kupata mbili za mkwezi nilimuuliza kulikoni kufanya vile?
Alinieleza kuwa kutokana na ugumu wa shughuli zake zimemfanya apungue uwezo wa kuangusha madafu mfululizo. Kama dafu la kwanza angelipasulia ndani asingeweza kunifurahisha kwa vile mnazi usingeweza kusimama tena.
Ile ilinikumbusha bwana mmoja akimwaga mzigo basi hulala kama bata haendelei tena.  Siku nyingine nilipokutana na yule bwana naye nilimuomba ajaribu mtindo ule kwa dafu la kwanza kulipasulia nje, alipofanya vile nilishangaa aliweza kuendelea na safari kwa kuweza kunipa raha ambazo nilikuwa nikizikosa siku za nyuma kwa kuwahi kufika kisha kulala kama bata.
Nina imani nimeeleweka kama una matatizo ya kufika haraka na ukifika uendelei na safari basi jaribu tiba hii ya bure ili mpenzi aufaidi mnazi wako na kufurahia utamu wa maji ya dafu.
Kwa leo inatosha tukutane wiki ijayo ni mimi Anti Nasra Shangingi Mstaafu