‘Hii ni pamoja na madereva wa magari kukosa umakini wa kufuatilia alama za barabarani kwa kuendesha mwendo kasi hata mahali penye makutano ya barabara ya gari na treni na hasa linalofanya safari zake ndani ya jiji la Dar ndiyo ambalo kwa sasa linahusisha vifo vya watu wengi kwa muda mfupi tangu kuanza kwa safari zake’ – Kamanda
Amesema mpaka sasa watu 8 wamekufa huku wengine wakijeruhiwa ambapo eneo hatari linaloongoza kwa matukio ya ajali ni Daraja la Buguruni kwa Mnyamani akitaja sababu kubwa wananchi wengi hujisahau na kukatiza juu ya reli kwa kuwa treni huwa halina breki za papo kwa papo basi hutokea vifo au majeruhi wengi yenye ulemavu wa kudumu pia’
Kamanda amesema’Polisi wa kikosi hiki wamekuwa wakipambana kikamilifu kuna siku walifanikiwa kukamata mabegi yaliyowekea bangi ambapo mtuhumiwa alifikishwa mahakamani, Polisi hawo pia waliwahi kumbaini mhalifu mmoja aliyekuwa na amebeba silaha isivyo halali ndani ya treni ambaye alikurupuka na kuitelekeza silaha hiyo’
Hii stori imeandikwa na gazeti la Mwananchi.