STAA wa kitambo kwenye filamu za Kibongo, Blandina Chagula ‘Johari’
amenaswa akipiga mitungi kwa sana ikiwa ni sehemu ya kufurahia uongozi
mpya wa Klabu ya Bongo Movie Unity.
Tukio hilo lilitokea wikiendi iliyopita katika Viwanja vya Leaders
Club, Kinondoni, Dar ambapo uchaguzi wa safu mpya ya uongozi wa klabu
hiyo ulimalizika na matokeo kuwatangaza mwenyekiti mpya Steven Mengele
‘Nyerere’ na wenzake kuwa washindi.
Katika mahojiano na mwandishi wetu, Johari alisema: “Kwa upande wangu
ninawaamini viongozi wote waliochaguliwa katika kutuletea maendeleo
katika klabu yetu kwa kufanya kazi kwa umoja na mshikamano. Wote
nawaamini na kusema kweli, hawa ndiyo viongozi tuliokuwa tunawataka.”
Katika uchaguzi huo, nafasi ya Makamu Mwenyekiti ilikwenda kwa
Mahsein Awadh ‘Dk. Cheni’, Katibu Mkuu Willium Mtitu, Katibu Msaidizi
Devotha Mbaga, Mweka Hazina Issa Mussa ‘Cloud’ na msaidizi wake Sabrina
Rupia ‘Cathy’