Saturday, 4 January 2014

BREAKING NEWS !!! MOTO WATEKETEZA NYUMBA ZAIDI YA 10 PEMBA.

Habari zilizotufikia hivi punde ni kwamba moto mkubwa umeteketeza nyumba zaidi ya 10 huko Pemba Micheweni. Jitihada za kuzima moto huo mpaka tunakwenda mitamboni zilikuwa zinaendelea, taarifa zimeeleza hakuna mtu hata mmoja aliyedhurika na moto huo.



Habari zimesema moto huo ulioanza mapema mchana, haijajulikani chanzo chake mpaka sasa, inadaiwa nyumba zaidi ya 10 zimeteketea ikiwa ni pamoja na mali ambazo thamani yake haikuweza kufahamika mara moja.

Jitihada za kumpata Sheha wa eneo hilo ili kutoa maelezo zaidi hazikuzaa matunda kwani hakuwa anapatikana hata kwenye simu yake. CHANZO jumamtanda blog